16 Feb, 2022

Kongamano la siku moja

Sera ya elimu ya mwaka 2006 haijafafanua vya kutosha juu ya elimu ya maandalizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ni nafasi kwa jamii kutoa maoni ili yaingizwe kwenye sera mpya mchambuzi sera Nassor Saleh Majid kwenye Kongamano la siku moja.
10 Feb, 2022

Head of development co-operation of the embassy of Ireland in Tanzania Mags Gaynor visits

The Irish Embassy visited Pemba Association of Civil Society Organizations earlier today to hear women talk about how they have become aware of land tenure rights and procedures and are spreading the word.

Head of development co-operation of the embassy of ireland in Tanzania Mags Gaynor with the beneficiaries of the land resource ownership project at PACSO office in Chake Chake Pemba where she expressed his satisfaction with its implementation.

6 Feb, 2022

Mafunzo ya waalimu

Mafunzo ya waalimu pamoja na maslahi yao yaingizwe kwenye sera mpya ijajyo ili kukuza kiwango cha elimu hapa Zanzibar Muwasilishaji Siti Makame Ali kwenye mkutano wa siku moja wa uchechemuzi wa sera ya elimu Zanzibar ya mwaka 2006 na kupata sera mpya.

 

Mkutano na wadau wa wilaya ya Mkoani Pemba wa kukusanya maoni juu ya sera ya elimu zanzibar ya mwaka 2006 katika ukumbi maktaba Chake chake Pemba leo tarehe 06/02/2022 chini ya ufadhili wa @FCSTZ.
16 Dec, 2021

PACSO: Yawanyooshea kidole wanaume vizingiti kwa wanawake kumiliki mali

MTANDAO wa Asasi wa Kiraia Pemba ‘PACSO’ umesema hakuna kanuni, sera, sheria wala mkataba wowote wa kitaifa, kikanda na wa kimataifa, unaomzuia mwanamke kutomiliki mali, bali kinachofanyika na kutengenezewa vikwazo na baadhi ya wanaume.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa mtandao huo, Mohamed Ali Khamis, wakati alipokuwa akifungua kongamano la siku moja la wanawake, kumiliki rasilimali lililoandaliwa na PACSO kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland, kupitia shirika la misaada la ‘IRISH AID’ na kufanyika Kiwanda cha Makonyo Wawi Chake chake.

Alisema, kama wanaume ambao ndio wanaoaminiwa na wanawake wataendelea kuzikalia haki za wanaweke, kundi hilo litaendelea kusikia kwenye vyombo vya habari, suala la umiliki wa rasilimali.

Mwenyekti huyo alisema, majukwaa kama hayo wakati mwengine huwasaidia wanawake kuwazindua na kupata uwelewa wa kuweza kudai haki zao mbali mbali.

“Wanawake wanahaki pia ya kumiliki rasilimali kama vile ardhi, lakini sasa kama wanaume hawakuwa tayari kujivua gamba, haki hiyo itaishia kwenye karatasi pekee,’’alieleza.

Mapema Mratibu wa miradi kutoka ‘PACSO’ Mohamed Najim Omar, alisema mradi huo ambao ni wa miezi miwili, unamalengo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kongamano kama hilo.

Shughuli nyingine wanayotarajia kuifanya, ni mafunzo kwa jamii juu ya elimu ya ushawishi na utetezi, wa masuala ya kumiliki rasilimali kwa wanawake.

Aidha Mratibu huyo alifafanua kuwa, pia wanatarajia kuwafunza wananchi masuala ya sheria na kanuni za ardhi, ili wapate uwelewa.

“Ni kweli kwenye suala la sheria za ardhi nako kuna mambo kadhaa, lakini ndani ya utekelezaji wa mradi huu, wananchi wakiwemo wanawake, watafunzwa sheria hizo,’’alieleza.

Akiwasilisha mada ya haki umiliki wa ardhi kwa wanawake, Kaimu Mratibu wa Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, alisema changamoto kubwa moja ni urasimu wa umiliki wa ardhi.

Jengine alisema, wanawake waliowengi hawana uwelewa mpana wa masuala ya sheria ya ardhi, hali inayopelekea kupoteza umiliki wa matumizi kwa njia rahisi.

Wakichangia mada hiyo wanakongamano hilo, walishauri elimu zaidi itolewe hasa kwa wanawake walioko vijijini, ambako ndio kwenye migogoro mingi ya ardhi.

Said Amour Juma wa Wawi, alisema kubwa zaidi la kuangalia ni uwelewa wa wananchi ikiwa uko vizuri, kwenye suala la umiliki.

Nuru Ali Nassor alisema, kwa vile suala la ucheleweshaji mirathi huchangia wanawake kukosa umiliki, ni vyema jamii ikafuata maelekezo ya kurithi kwa wakati.

Kwa upande wake, Shikha Kitwana Sururu, aliziomba mamlaka husika, kuwasaidia zaidi wanawake hasa wanyonge ili wasipoteze haki zao za umiliki.

Hata hivyo mshiriki Fatma Khamis Juma, alipendekeza liwepo somo maalum la urithi kuanzia elimu ya msingi, ili jambo hilo lifahamike vyema ndani ya jamii.

“Lakini hata suala la ushirikina uliyopo ndani ya jamii na vitisho vya wanaume, wakati mwengine, huwa unatujenga woga sisi kudai haki zetu mfano za urithi,’’alifafanua Zamzam Khamis Saburi wa Kengeja.

Mradi huo wa kuwajengea uwezo wanawake kuweza kudai rasilimali zao kama vile ardhi, ni wa miezi miwili unatekelezwa na PACSO kwa ufadhili wa shirika la misaada la Ireland ‘IRISH AID’.