MKUTANO WA UZINDUZI WA UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA (PETS) ULIOWASHIRIKISHA VIONGOZI WA SERIKALI ,ASASI ZA KIRAIA,WAADISHI WA HABARI NA WADAU WENGINE KUTOKA KATIKA WILAYA YA MKOANI NA CHAKE CHAKE PEMBA.

Asasi isiyo ya kiserikali PACSO ilifanya Mkutano wa uzinduzi wa mradi wa ufuatiliaji wa rasilimali za umma (PETS). Uliowashirikisha viongozi wa serikali, Asasi za kiraia ,waandishi wa habari, wadau wengine kutoka katika wilaya ya mkoani na chakechake. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa GREEN FOLIAGE HOTEL. iliopo mgogoni chakechake mkoa wa kusini Pemba, siku ya Jumamosi tarehe 25/7/2020. saa 3:00 asubuhi. Mkutano huo uliwapa watu fursa ya kuchangia maoni yao mbalimbali kuhusiana na mada ya ufuatiliaji wa rasilimali za umma (PETS).

 

 Wadau walichangia mapendekezo yafuatayo;

  • Wachukuliwe watu ambao wanaujuzi kulingana na masuala ya ufuatiliaji.
  • Watu wasiwe wanafanya kazi kimazoea.
  • Waweko watu ambao watafanya kazi kwa umakini bila ya kuhofia kutoa kitu chochote kibaya .
  • Wawekwe watu katika kamati ambao wapo tayari kujitolea.
  • Mradi uendane na taasisi husika.
  • Mradi umalizike kwa mda husika .

 

Mratib wa asasi za kiraia Pemba, nae aliipongeza PACSO kwa kuweza kujitolea kushirikiana na serikali katika suala la ufuatiliaji wa rasilimali za umma.PACSO ni asasi inayofanya vizuri katika kuhakikisha miradi yao inamalizika kwa ubora zaidi. Aidha aliwashauri watu wawe tayari katika kutoa maoni yoyote yale na kutoa mchango wowote ule ili mradi ukamilike vizuri na pia aliwashauri PACSO  wawe tayari katika kupokea ushauri utakao tolewa.