Mkutano wa pili Zanzibar (PACSO na ZACPO) uliowashirikisha wadau mbalimbali ili kujadili mfumo mzima wa uendeshaji wa zao la karafuu Zanzibar.

Asasi za kiraia Zanzibar PACSO na ZACPO walikutana na wadau wa zao la karafuu visiwani Pemba katika ukumbi wa GREEN FOLIAGE HOTEL .Siku ya jumapili tarehe 28/6/2020 muda wa saa 3:00 asubuhi kisiwani Pemba katika wilaya ya chakechake mkoa wa kusini Pemba. Walijadili mada ya kujenga nguvu ya pamoja na asasi za kiraia kuhusiana na utetezi wa wakulima wa karafuu. Mkufunzi aliwasilisha mada ya kujenga nguvu ya pamoja na asasi za kiraia kuhusiana na utetezi wa wakulima wa zao la karafuu.

Baadae washiriki walipata fursa ya kuchangia mjadala huo vile vile wakatoa maoni yao kuwa kuna haja ya kuwa na nguvu ya pamoja kupitia zao hilo la karafuu.

 

Miongoni mwa mdau wa zao la karafuu akitoa maoni yake  kuhusu mada ya kujenga nguvu ya pamoja na asasi za kiraia kuhusiana na utetezi wa wakulima wa karafuu kisiwani pemba. Alitoa maoni yake kuwa kuna haja ya kuwa na nguvu ya pamoja kupitia zao hilo la karafuu.