Mkutano ulio washirikisha PACSO na ZACPO pamoja na wakulima ili kujadili mfumo mzima wa uendeshaji wa zao la karafuu Zanzibar.

Wahusika wa asasi za kiraia Zanzibar (PACSO na ZACPO) wakishirikiana na wakulima wa zao la karafuu kisiwani Pemba. siku ya Alhamis tarehe 02/6/2020 katika ukumbi wa GREEN FOLIAGE HOTEL. muda wa saa 3:30 asubuhi walijadili athari zinazotokana na bei ya karafuu kuwa ni bei ambayo ipo katika mfumo mmoja tu waserikali (monoloy cloves industry). Mada hii iliwasilishwa na wakufunzi wawili ambao mmoja ni mtu aliyefanya tafiti ya zao la karafuu kisiwani Pemba na mkufunzi mwengine aliongelea kuhusu masuala ya sheria kuhusu zao hilo la karafuu , hata hivyo wachangiaji walipata fursa ya kuchangia mada hio.Hivyo mjadala huo uliibua hisia tofauti na mwisho wake  walitoa rai zao kuwa kuna baadhi ya sheria zifanyiwe mapitio rafiki ili ziwe rafiki kwa wadau.